Pages

Monday, October 21, 2013

Wanafunzi wapambana na polisi Cairo



131006171033_cairo_clashes_ap_304x171_ap_nocredit_5d596.jpg
Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili huku wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa, pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi miwili iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.

No comments:

Post a Comment