Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimkabidhi zawadi ya ngao
Balozi wa Marekani Nchini aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt
(kulia) kwa ushirikiano wake aliutoa kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi wakati wa uongozi wake nchini. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Malimi Malemi. Waziri Nchimbi pamoja na
Watendaji Wakuu wa wizara yake walimuaga balozi huyo katika Ukumbi wa
Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiteta jambo na
Balozi wa Marekani nchini aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt kabla
ya hafla fupi ya kumuaga balozi huyo aliyemaliza muda wake wa uongozi
nchini. Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa wizara yake
walimuaga balozi huyo katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini
Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia waliokaa),
Balozi wa Marekani nchini aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt (wa
pili kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mbarak Abdulwakil (kulia), Naibu Balozi wa Marekani nchini, Virginia
Blaser (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Malimi Malemi (wane
kulia waliosimama) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla fupi ya kumuaga
Balozi Lenhardt. Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa wizara yake
walimuaga balozi huyo katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini
Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
No comments:
Post a Comment