Askari polisi akiwa akichukua maelezo kwa majeruhi kwenye wodi ya wanau
Watu 17
wamejeruhiwa baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kutoka ulowa
kwenda mjini kahama kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha
Nyandekwa wilaya ya kahama mkoani Shinyanga.
Ajali
hiyo imetokea leo asubuhi ikilihusisha gari namba T 208 AGE lilokuwa
likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina la Rashid Ramadhan mkazi wa
Kahama mjini, ambaye hata hivyo alitoroka baada ya tukio hilo.Kwa mujibu
wa daktari mfawidhi wa hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga,
jumla ya majeruhi 5 wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa huku 12 wakiwa
wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.
Mganga mfawidhi wa hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga akiongea na waandishi wa habari
Daktari
Nyaga amewataja waliolazwa kuwa ni Elizabert Mgesa (49), Katarina Makoye
(32), Eliza Timotheo (30), Ngeke Chanila (23), Zawadi Andrea (18), Amos
Hussein (32) na Adam John (20) ambaye alikuwa kondakta wa gari
hilo.Wengine ni Zakaria Leonce (25), Mabala Paulo (28), Hamis Makala
(26), John Marcel (26) na Michael Rashid (47) na motto benad Paulo
mwenye umri wa miezi mitano na kwamba wote hali zao zinaendelea
vizuri.Jeshi la Polisi wilayani kahama limethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kwamba uchunguzi wakubaini chanzo chake unafanywa, huku juhudi
za kumtafuta dereva wa gari hilo zikiendelea.
Ajabu sana: Majeruhi wawili wakiwa katika kitanda kimoja
Mama aliyejeruhiwa pia katika ajali hiyo
Mgonjwa akiwa amepumzika baada ya kupatiwa huduma
Miongoni mwa waliopata ajali akiwa kitandani wodini
Dada huyu akiwa ametulia kitandani kumuomba mungu ampe ahueni
Majeruhi wawili katika kitanda kimoja kama inanvyoonekana
No comments:
Post a Comment