Klabu ya Al Ahly ya Misri imeshinda taji la klabu bingwa Afrika ilipoicharaza Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa mabao 2-0 katika mkondo wa pili na wa mechi ya mwisho mjini Cairo Jumapili.
Ahly, waliojinyakulia kombe hilo kwa mara ya saba walipata alama 3-1 kwa ujumla.
Taarifa zinazohusianaAfrika, Michezo
Kulikuwa na ripoti za vurugu kuzuka kati ya mamia ya wafuasi wa Ahly na polisi nchini Misri, kabla ya mchuano kuanza.
Kulikuwa na ripoti za vurugu kuzuka kati ya mamia ya wafuasi wa Ahly na polisi nchini Misri, kabla ya mchuano kuanza.
Pindi
vurugu zilipositishwa , mchezaji gwiji, Mohamed Aboutrika ndiye
aliyeingiza bao la kwanza katika dakika ya 54. Ahmed Abdul Zaher
aliingiza bao la pili kwa Ahly katika dakika 78.
Hata
hivyo mabingwa wa Misri walipungua kwa mtu mmoja na kusalia 10 dakika
sita baada ya difenda Sherif Abdel Fadil kuondolewa uwanjani kwa
kumfanyia masihara Daine Klate.
Pirates,
waliibuka mabingwa mwaka mwaka 1995, walicheza kadri ya uwezo wao,
lakini waliondokewa na matumaini Ahly walipoingiza bao lao la pili
katika uwanja uliokuwa umesongamana watu mjini Cairo.
Hata hivyo mabingwa hao wa Afrika Kusini walikosa nafasi kadhaa za kuingiza bao.
Ahly wamepata kombe hilo pamoja na kitita cha dola milioni moja na nusu
Pia watawakilisha Afrika katika kombe la dunia la klabu bingwa duniani litakalofanyika nchini Morocco mwezi ujao.
Mamia ya
mashabiki wa Ahly walikabiliana na polisi kabla ya mechi kuong'oa nanga.
Ni mechi ya kwanza kubwa ambako mashabiki wameruhusiwa kuingia uwanjani
tangu watu 74 wengi waliokuwa mashabiki wa Al Ahly , waliuawa katika
mechi iliyokumbwa na vurugu mwaka jana.
Polisi
wlailazimika kutumia gesi ya kutoa machozi, kuwatawanya mashabiki
waliokuwa wanatupia mawe huku wakiingia kwa lazima ndani ya uwanja.
No comments:
Post a Comment