Hapa ndipo wanapoishi watu hawa baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Watoto wakiwa michezoni huku wasijue watalala wapi ukifika usiku
Ni majonzi makubwa
Hizi ndizo nyumba zao , wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba zao kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka majangili nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo na kusababisha maelfu ya wanakijiji kuishi chini ya miti
Mzee na binti yake wakiwa wanaondoka wanaondoka
Wakina mama wakiwa wanafungasha
Wakubwa kwa watoto wakiwa wanakihama kijiji hicho
Wakiendelea kuhama kijijini hapo
Wakazi wa kijiji cha Kabage wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa wanaishi chini ya miti na familia zao baada ya nyumba zao kuchomwa moto na askari waliokuwa wanafanya oparesheni majangiri wiki iliyopita jumla ya zaidi ya kaya 500 zilichomewa nyumba kijijini hapo na kuleta malalamiko ya wanakijiji hao kwa kile wanachodai kijiji hicho ni halali na kimesajiliwa kisheria toka mwaka jana na kupewa usajili wenye namba KT/KIJ/47 Hawana makazi tena hawa
Mtoto akiwa amelala huku akiwa hana pa kuhifadhiwa ikiwa nyumba yao imechomwa moto
Mchungaji wa kanisa la PAG wa kijiji cha Mwamkulu Petro Mahenga akimfariji mmoja wa wahanga waliochomewa nyumba zao katika kijiji cha kabage wilayani Mpanda Daudi Belehiwa ambae pia mke wake aitwae Kurwa Elias alijifungua mtoto ambae hajatimiza miezi yake kutokana na kutembea kwa muda mrefu wakati akiwakimbia askari hao hata hivyo mtoto huyo aliezaliwa akiwa na miezi nane alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa. Vyombo vikiwa havina pa kupelekwa
Dogo akiwa ameishiwa Nguvu
Inasikitisha sana Wanakijiji hawa hawana makazi sasa
Na Walter Mguluchuma-Kativi yetu
Na Walter Mguluchuma-Kativi yetu
Mpanda
Askari waliokuwa wanafanya operesheni ya kuwasaka
majangili waliokuwa wakiongozwa na JWTZ wamelalamikiwa kwa kuchoma
nyumba za wanakijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na
kuwasababishia wananchi wa kijiji hicho kuishi chini ya miti na
akina mama kujifungua kabla ya wakati
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Maganga Kasope alisema tukio
hilo lilitokea hapo Oktoba 28 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi na
kusababisha zaidi ya kaya mia sita kukosa makazi ya kuishi
Alisema kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya elfu kumi ni
kijiji halali kwani kalisajiliwa toka mwaka jana na kupewa usajiri
wenye namba za usajiri wa kijiji KT/KIJ/47 hivyo wameshangazwa na wakazi
wa kijiji hicho kuchomewa nyumba zao wakati ni kijiji halali
alisema kuwa katika tukio hilo akina mama watatu ambao
walikua wajawazito walilazimika kujifungulia kwenye mbuga za mpunga
wakati wakikimbia kuelekea kijiji cha jirani cha mwamkulu kujihifadhi
hivyo kutokana kutembea kwa umbali mrefu hivyo ililazimika kujifungulia
njiani na kujifungua watoto wakiwa salama
Kwa upande wake mhanga wa tukio hilo Daudi Lulehiwa 28 alisema kutokana na tukio hilo iliwalazimu ketembea umbali mrefu kwa ajiri ya kukimbilia katika kijiji cha jirani cha Mwamkulu huku wakiwa wamebeba mizigo yao na iliwalaziri hata watoto wao wadogo kutembea kwa miguu umbali huo mrefu
Alisema mkewe aitwaye Kulwa Elias 24 ambae alikuwa ni
mjamzito wa miezi minane kutokana na kutembea umbali huu huku akiwa
amebeba mizigo aliweza kujifungua mtoto wa wakike ambae alikuwa sio
ridhiki na alifariki muda mfupi baada ya kujifungulia chini ya mti
Nae mchungaji wa Kanisa la wa Kanisa la P.A.G wa Kijiji
cha Mwamkulu Mchungaji Petro Mahega alisema toka wahanga hao
waliokimbilia kijijini hapo wamekuwa wakiishi kama wanyama wao na
familia zao
Alieleza kutokana na wahanga hao kuishi chini ya miti na
mbaya zaidi hapo juzi walinyeshewa na mvua ambayo ilinyesha majira ya
usiku hivyo ametowa jengo la Kanisa lake igawa ni dogo sana litumike kwa
ajiri ya kuwahifadhi wahanga hao
Kwa upande wake mhanga mwingine Malidadi Gwachele 72 ambae anaishi na familia yake ya watu 20 wakiwa chini ya mtu alieleza kuwa wameanza kuhathirika kwa kupata magonjwa ya kuharisha
Alisema hari hiyo imesababishwa na maji wanayo kunywa na
mazingira wanayoishi na hasa watoto wadogo ndio wanao athirika zaidi
za magonjwa hayo
Mdae
Masanja alisema mbali ya kuchomewa nyumba yake pia amepoteza chakula
chake ambacho kiliteketea kwa moto baada ya kushindwa kukihamisha kwenye
nyumba yake wakati ikiungua
Alisema sasa hivi wanalala nje bila hata kujali jinsia
za familia walizo nazo kutokana natukio lenyewe inawalazimu walale hivyo
na wamekuwa wakijisaidia kwenye vichaka
Aidha Mhanga Katali Ngeleja alieleza mbele ya mwandishi
wa habari hizi ambae alitembelea eneo hilo kuwa wako watoto wenye umri
kati ya miaka saba na nane walipotezana na familia zao kwa muda wa siku
mbili
Alieleza yupo pia mwenzao mmoja ambae alikuwa anamiliki
mashine ya kusanga unga iliteketea kabisa kwa moto ikiwa ndani ya
kibanda cha nyumba
No comments:
Post a Comment