Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 6, 2013

BAYERN MUNICH NA MANCHESTER CITY ZAFUZU HATUA YA 16 BORA LIGI YA MABINGWA.


 Robin van Persie alikosa mkwaju wa penalti na kiungo Marouane Fellaini akilimwa kadi nyekundu huku Manchester United ikijiweka kwenye nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora pale ilipolazimishwa sare ya bila kufungana na Real Sociedad.
Paris St Germain walilazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani na Anderlecht ya Ubelgiji kwenye mchzeo wa kundi C.
Wageni walitangulia kufunga dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Demy De Zeeuw kabla ya Zlatan Ibrahimovic hajafunga bao la kusawazisha dakika mbili baadae.


Real Madrid walinyimwa nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Champions League hapa jana  usiku baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 d kwenye mchezo wa kuvutia dhidi ya Juventus.
Ushindi nchini Italia ungeivusha Real Madrid kwenye hatua inayofuata.
Sare ya jana imewapa matumaini Juventus ya kufuzu kutoka kundi B hasa baada ya FC Copenhagen kuifunga Galatasaray 1-0.

Mario Mandzukic aliifungia bao pekee Bayern Munich kwenye ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Plzen,ushindi huo uliakikishia nafasi Bayern kufuzu hatua ya mtoani  wa 1-0 on Tuesday night to claim their place in the knockout stages of the Champions League.
Alvaro Negredo alifunga hat-trick,Sergio Aguero akafunga mabao mawili kwenye mchezo ambao Manchester City iliitandika CSKA Moscow mabao 5-2 na kukata tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment