SHIRIKISHO
la Soka Duniani-FIFA, limethibitisha kupata malalamiko kutoka
Shirikisho la Soka la Burkina Faso kuhusiana na mchezo wao wa kufuzu
michuano ya Kombe la Dunia ambapo nchi hiyo ilifungwa bao 1-0 na
Algeria. Maofisa hao wa Burkinabe wameiandikia FIFA kulalamikia baadhi
ya maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi Badara Diatta wa Senegal wakati wa
mchezo huo, maamuzi ambayo yalipelekea kukataliwa kwa bao lao katika
kipindi cha kwanza.
Shirikisho
hilo pia limelalamikia kadi ya njano aliyopewa nahodha wa Algeria
Madgid Bougherra wakidai kuwa alistahili kadi nyekundu baada ya
kumfanyia madhambi nahodha wa Burkinabe Charles Kabore katika eneo la
hatari. Uamuzi wa FIFA unatarajiwa kuhusiana na tukio la mchezo huo
unatarajiwa kutolewa Desemba 5, siku moja kabla ya ratiba kamili ya
Kombe la Dunia
No comments:
Post a Comment