Dar
es Salaam, Tanzania.Naibu Katibu Mkuu na Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo
wameuandikia barua uongozi wa juu wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Wilbrod Slaa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe watoe maelezo kuhusu ripoti ya kuwachafua mitandaoni.
Zitto na Dk Mkumbo wanatuhumiwa kupokea fedha na kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuiua Chadema.
Ripoti hiyo imesambaa kwenye
mitandao ya kijamii ikidaiwa kuandaliwa na Kitengo cha Upelelezi cha
Chadema kwa ajili ya kufuatalia mwenendo wa Zitto kuanzia mwaka 2008.
Katibu Mwenezi wa Chadema, John Mnyika ameikana ripoti hiyo na kueleza kuwa haijaandaliwa na makao makuu ya Chadema.
Mnyika amebainisha kwamba Zitto ameibua jambo ambalo anafahamu kuwa limeshughulikiwa na uongozi wa cha hicho.
"Zitto anajua kuwa Andrea
Cordes aliniandikia barua pepe na nakala kwake, nikawajibu kwamba ripoti
hiyo hajaandikwa na makao makuu ya chama na tukipokea malalamiko rasmi
tutachunguza kwa sasa chama kinachukulia ripoti hiyo kama ripoti
nyingine zinazosambazwa mitandaoni," amesema Mnyika.
Soma hapa taarifa kwa vyombo
vya habari ambayo Zitto ameutaka uongozi wa Chadema kutoa maelezi kuhusu
taarifa iliyosambazwa mitandani kwamba anaivuruga Chadema
No comments:
Post a Comment