Mwanasheria Mkuu wa Chadema,Tundu Lissu akionyesha waraka aliodai kuwa
ni orijino badala ya ule uliosambazwa kwenye mitandao na kwenye vyombo vya
habari aliodai kuwa ni feki,kushoto ni John Mnyika na Mbunge wa Ubungo na
Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi Wilfred Lwakatare
WAKATI Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), ikipinga waraka uliosambazwa kwenye vyonbo vya habari
na katika mitandao mbalimbali kuwa ni feki ila walionao ndiyo orijino,Chama
hicho leo hii kimetangaza mchakato wa kuanza kwa Uchaguzi Mkuu wa ndani,
kuanzia balozi wa nyumba kumi hadi ngazi ya Mwenyekiti wa Chama Kitaifa.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari leo jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu
amesema kwamba mchakato wa uchaguzi huo uta anza rasmi January mwaka 2014 na
kukamilika Juni.Hatua ya Chadema kutangaza kuanza kwa uchaguzi huo ni sawa na
kujibu hoja iliyokuwa katika waraka uliosababisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama
Zitto Kabwe na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Dk Kitilia Mkumbo kuvuliwa
nyadhifa zao zote ndani ya Chama.Kwa muujibu wa waraka huo
ambayo Lissu amesema kwamba ni feki wahusika walidai kwmaba lengo la kwanza
ilikuwa ni kuandaa mpango mkakati wa kuilazimisha Chama hicho kufanya Uchaguzi
Mkuu kutokana na viongozi wake kukwepa uchaguzi huo mara kwa mara.
Katika
hatua nyingine Zitto na Mwenzake Dk Kitilia wamepewa hati ya mashtaka ya tuhuma
zao yenye tuhuma 11 kila mmoja, ambazo wanatakiwa kuyajibu kwa maandishi ndani
ya siku 14 kabla ya kuitwa katika Kamati Kuu kwa kujieleza kabla ya maamuzi ya
ama wafukuzwe ama wasifukuzwe kufanyika
Na Habari Mpya
No comments:
Post a Comment