Pages

Tuesday, November 26, 2013

Chadema,watangaza Uchaguzi Mkuu


Mwanasheria Mkuu wa Chadema,Tundu Lissu akionyesha waraka aliodai kuwa ni orijino badala ya ule uliosambazwa kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari aliodai kuwa ni feki,kushoto ni John Mnyika na Mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi Wilfred Lwakatare
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikipinga waraka uliosambazwa kwenye vyonbo vya habari na katika mitandao mbalimbali kuwa ni feki ila walionao ndiyo orijino,Chama hicho leo hii kimetangaza mchakato wa kuanza kwa Uchaguzi Mkuu wa ndani, kuanzia balozi wa nyumba kumi hadi ngazi ya Mwenyekiti wa Chama Kitaifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba mchakato wa uchaguzi huo uta anza rasmi January mwaka 2014 na kukamilika Juni.Hatua ya Chadema kutangaza kuanza kwa uchaguzi huo ni sawa na kujibu hoja iliyokuwa katika waraka uliosababisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zitto Kabwe na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Dk Kitilia Mkumbo kuvuliwa nyadhifa zao zote ndani ya Chama.Kwa muujibu wa waraka huo ambayo Lissu amesema kwamba ni feki wahusika walidai kwmaba lengo la kwanza ilikuwa ni kuandaa mpango mkakati wa kuilazimisha Chama hicho kufanya Uchaguzi Mkuu kutokana na viongozi wake kukwepa uchaguzi huo mara kwa mara.

Katika hatua nyingine Zitto na Mwenzake Dk Kitilia wamepewa hati ya mashtaka ya tuhuma zao yenye tuhuma 11 kila mmoja, ambazo wanatakiwa kuyajibu kwa maandishi ndani ya siku 14 kabla ya kuitwa katika Kamati Kuu kwa kujieleza kabla ya maamuzi ya ama wafukuzwe ama wasifukuzwe kufanyika
Na Habari Mpya
                       CLICK HAPA LIKE PAGE YETU KWA NEWS UPDATES ZA KILA SIKU

No comments:

Post a Comment