Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi leo
asubuhi amepelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Dk. Mvungi
alijeruhiwa vibaya na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi usiku wa
Novemba 2 mwaka huu nyumbani kwake, Kibamba jijini Dar es Salaam na
alikuwa akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
katika kitengo cha MOI.
No comments:
Post a Comment