Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 26, 2013

Dr. Kitila Mkumbo azikataa salamu za pole toka kwa Mwigulu Nchemba kwa madai kuwa ni mnafiki



Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Kitila Mkumbo, amemshambulia kwa maneno na kumrushia vijembe Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, kuwa kauli ya kumpa pole baada ya kusikia amevuliwa uongozi ni kiherehere.
 Dk. Kitila alitoa kauli hiyo juzi mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Saalam, baada ya kutoa tamko lake kufuatia hatua ya chama chake ya kumvua nafasi za mamlaka ndani ya Chadema.
 
 “Nimeshangaa kusikia Nchemba ananipa pole ilihali hakuna siku aliyowahi kunipongeza, mara zote amekuwa akisema usomi wangu ni wa ovyo… hiki kuherehere cha kunipa pole kimetoka wapi?” alihoji Dk. Mkumbo.
 
 Alisema pamoja na kiherehere hicho cha Nchemba, bado msimamo wake ni dhahiri kwani mwaka 2015 ukifika atapambana naye iwe akiwa mwanachama wa Chadema au vinginevyo.
 
 “Napenda kumtumia salama kuwa niwe mwanachama nisiwe, niwe Chadema au nje ya Chadema, ajue lazima nimng’oe kwenye uchaguzi mkuu ujao hakuna mchezo kwenye hilo, nimedhamiria,” alisisitiza Dk. Kitila.
  Nchemba amekuwa akituhumiwa na Chadema kwa kuwatunia wanachama kadhaa ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya kukisaliti chama pamoja na waliofukuzwa kutokana na tuhuma kadhaa.
                       CLICK HAPA LIKE PAGE YETU KWA NEWS UPDATES ZA KILA SIKU

No comments:

Post a Comment