Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 28, 2013

EBSS: Yamkutanisha Emmanuel Msuya na kaka zake ambao hakuwahi kabisa kuwaona, zifahamu nyimbo 5 binafsi za washiriki




Wakati watu wengi wanazimulika zaidi million 50 atakazopewa mshindi wa shindano la kuimba la EBSS 2013, mshiriki namba 21 wa shindano hilo Emmanuel Msuya amefaidika kijamii pia na ameiandika historia ya maisha yake kupitia shindano hilo kwa kuwa limemkutanisha na kaka zake wa damu moja ambao hakuwahi kabisa kuwaona.
Emmanuel Msuya ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa hakuwahi kabisa kuwaona kaka zake ambao wameshare baba mmoja, na kwamba alikuwa ameshakata tamaa lakini walipomuona kwenye shindano hilo walimfuata wenyewe.
“EBSS imenifaidisha sana, nimeweza kukutana na kaka zangu ambao nilikuwa siwajawahi kuwaona tangu nimezaliwa. Ni kaka zangu wa damu...baba mmoja ila mama ndio tofauti.”Msuya ameiambia tovuti ya Times Fm.
Akieleza jinsi alivyokutana nao, Emmanuel Msuya amesema kaka zake walimuona kwenye TV ndipo wakaamua kumfuata kambini na kwa mara ya kwanza akaonana nao.
“Waliponiona kwenye TV wakaja pale Mama Afrika na ndipo kwa mara ya kwanza tukaweza kuonana.” Ameeleza.
Katika habari nyingine, nyimbo binafsi za washiriki watano wa EBSS 2013 zimeshatoka tayari ambapo washiriki hao wamerekodi katika studio tofauti tofauti na producers wakubwa.
Wimbo wa Emmnanuel Msuya unaitwa ‘Leo Leo’ ambao uko katika mahadhi ya Kiafrika na umepikwa na Shedy Clever.
Amina Chibaba amerekodi wimbo unaitwa ‘Subira ya Moyo’ huku Melisa John amerekodi wimbo unaitwa Ah Ah, uliofanywa na Lamar wa Fish Crab.
Maina Thadei yeye amerekodi wimbo wa tofauti zaidi wenye mahadhi ya Taarab unaoitwa ‘Panya Buku’.
November 30 mwaka huu pale Escape 1, mmoja kati ya washiriki hawa watano atatangazwa kuwa mshindi wa EBSS 2013.
Endelea kufuatilia hapa na sikiliza 100.5 Times Fm utazisikia nyimbo hizo tano.chanzo TIMES FM




No comments:

Post a Comment