Pages

Saturday, November 16, 2013

Exclusive: Steve Nyerere kufanya show London Uingereza, atafanya interview na BBC


Mchekeshaji aliyepata mafanikio kwa kuiga sauti ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maarufu kwa jina la Steve Nyerere anaendelea kupanda ngazi ya mafanikio kimataifa na kuvuka mipaka ya Afrika Mashariki na Afrika hadi kwa Malikia Elizabeth.
Steve Nyerere ameiambia tovuti ya Times fm exclusively kuwa kampuni ya Proin Entertainment inayosimamia kazi zake imempa deal ya kufanya show jijini London Uingereza.
Sio hayo tu, Muigizaji huyo amepata mualiko wa kufanya interview na kituo kikubwa cha television duniani cha Uingereza ‘BBC’.
“Kazi zangu zote zinasimamiwa na Proin, kazi zangu zote.. na vilevile tumefikia sehemu nzuri wameanza kunitangaza nje ya nchi. Kwa mfano sasa hivi nina show yangu London natarajia kwenda kufanya.” Amesema Steve.
“Nimepata bahati ya mwaliko mzuri wa kwenda kuhojiwa BBC, nadhani mwezi wa kwanza Mungu akibariki ntaenda. Kwa hiyo hivyo ni vitu ambavyo vitanitangaza mimi kama Steve Nyerere kwa sababu vizazi vinavyozaliwa vimeanza kusahau Mwalimu Nyerere ni nani. Kwa hiyo mimi ni jukumu langu kuwakumbusha mwalimu, kwa mwaka angalau movie moja ili kuleta kitu kizuri Tanzania.” Aliongeza.
Msikilize hapa.chanzo Timesfm

No comments:

Post a Comment