HATARI! VIJANA WAJIRUSHA BAHARINI KUTOKA JUU YA PANTONI KWENYE KIVUKO CHA KIGAMBONI DAR
Kijana
alionekana anaruka kutoka Juu ya Pantoni (Kivuko) mbele kidogo baada ya
Pantoni hiyo MV. Magogoni kuanza safari zake, huku abiria wengi wakiwa
wameacha viti vyao na kuendelea kushangaa.
PICHA ZOTE NA DAR ES SALAAM YETU
Wakati huo huo mwengine nae alionekana anachomokea kutoka katika Pantoni hiyo na kuzamia majini.
Wasafiri walipigwa butwaa
zaidi kuona kasi ya vijana hao inazidi kuongezeka na huyu kijanda ndiye
aliyekuwa anafunga dimba la kuzamia majini.
Ni zaidi ya Vijana 9 wote
walipanda Pantoni ya MV. Magogoni bila ulinzi wowote na baadae kupiga
mbizi wakitokea katika Pantoni hilo.
No comments:
Post a Comment