Wakati Naibu Spika, Job Ndugai akisema maelezo binafsi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) kuhusu
biashara ya dawa za kulevya na athari zake aliyoyatoa bungeni juzi jioni hayatajadiliwa, Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini kimeshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za hizo.
Ndugai
alitoa ufafanuzi huo jana baada ya Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi
Lugola kuomba mwongozo jana, akitaka Bunge likubali mjadala wa suala
hilo kutokana na unyeti wake.
Akizungumza
na Mwananchi Dar es Salaam jana, Kamanda wa kitengo hicho, Godfrey
Nzowa alisema wameshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa
dawa za kulevya, ambao sasa wanatumia barabara badala ya anga.
“Mfano
mzuri, tumeshtukia usafirishaji wa epedrine na Juni 24 mwaka huu, Saada
Ally Kilongo (26) alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere na kilo 11,000 za dawa za kulevya aina ya epedrine, ambazo ni
mali ghafi za thamani zaidi ya Sh170 mil,” alisema.
SOURCE:MWANANCHI
SOURCE:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment