Pages

Thursday, November 7, 2013

KESI YA SHEIKH PONDA YAPIGWA KALENDA


 Sheikh issa Ponda akiwa mahakamani leo
Kesi inayomkabili Katibu wa BAKWATA Sheikh Issa Ponda Imeairishwa tena Mpaka tarehe 21 Mwezi huu.Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro Ambapo sheikh Issa Ponda Anakabiliwa na Mashata matatu Imearishwa kutokana na jalada la kesi hiyo kuwa ,mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Mahakama imesema kwamba jalada ya kesi hiyo lilihitajika mahakama kuu tangu mwezo october na bado halijarudi.Kwa mujibu wa mahakama ya hakimu Mkazi mkoa wa morogoro imesema kesi hiyo itaendelea kutajwa mahakamani hapo mpaka jadala la kesi hiyo litakaoletwa.Kesi hiyo iliyokuwa ianze kusikilizwa lero  ambapo upande wa Mashtaka ulikuwa umejiandaa tayari kutoa ushahidi kuhusu kesi inayomkabili sheokh ponda.Sheikh Ponda amerudishwa Rumande.

CHANZO MATUKIO BLOG
Ulinzi mkali ulikuwa umemarishwa mahakamani hapo wakati sheikh Ponda alipofikishwa mahakamani leo lakini wafuasi wake wamejitokeza kwa uchache tofauti na kawaida yao.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa mahamakani hapo leo

No comments:

Post a Comment