Mrisho Ngassa akishangilia baada ya Said Morad kuisawazishia Stars,
Na Mahmoud Zubeiry, Machakos
TANZANIA
Bara, Kilimanjaro Stars imeanza taratibu michuano ya Kombe la Mataifa
ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kutoa sare ya 1-1
na mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia au Chipolopolo kwenye Uwanja wa
Kenyatta, Machakos, Kenya.
Katika
mchezo huo wa Kundi B, Zambia ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao
kupitia kwa Ronald Kampamba dakika ya 41, akiunganisha kwa kichwa krosi
ya Felix Katongo.
Zambia
walitawala zaidi mchezo huo kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi
zaidi ya nne za kufunga, lakini sifa zimuendee kipa Ivon Philip Mapunda
aliyeokoa michomo kadhaa ya hatari.
Kipindi
cha pili, Stars ilibadilika mno kiuchezaji, japokuwa wachezaji
waliomaliza kipindi cha kwanza ndiyo wote waliorejea kuanza ngwe hiyo ya
lala salama.
Kutokana
na mshambulizi mfululizo langoni mwa Zambia, Bara walipata kona dakika
ya 48 ambayo ilikwenda kuchongwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na
kuunganishwa nyavuni na Said Morad kwa kichwa.
Baada ya
bao hilo, Zambia walianza kuutafuta mpira kwa tochi na kama si umahiri
wa kipa wao, Nsabata Toaster kuokoa hatari nyingi, Stars wangeweza
kuondoka na ushindi.
Kwa
matokeo hayo, Burundi inaongoza kundi hilo baada ya kuifunga Somalia 2-0
katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo kwenye Uwanja huo.
Mabao ya Burundi yalifungwa na Abdoul Fiston dakika ya 40 na Nduwarugira Christopher dakika ya 55.
Mchezo wa pili wa Kundi B unatarajiwa kufanyika jioni hii kati ya Bara na Zambia kwenye Uwanja huo huo.
Kikosi
cha Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad,
Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano
‘Messi’ dk89, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias
Maguri/Haroun Chanongo dk72, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
No comments:
Post a Comment