Pages
▼
MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
Wabunge
wa CCM,Kangi Lugola (kulia) wa Jimbo la Mwibara,na Jenista Mhagama
(katikati) wa Jimbo la Peramiho,wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kushoto) walipokutana kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma bunge linaendelea na mkutano wa 13 mjini
humo ambapo hoja mbali mbali zinajadiliwa.
Mwenyekiti
wa Wabunge wa CCM,Mkoa wa Dar es salaam,Abasy Mtemvu (kulia) amabaye
pia ni Mbunge wa Temeke, na Idd Azan (kushoto) ambaye pia ni Mbunge wa
Kinondoni wakifurahia mchakato wa vikao vya bunge vinavyoendelea mjini
Dodoma walipokutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex
Msama(katikati) kwenye viwanja vya bunge.
Naibu
Waziri wa Fedha na uchumi, Saada Mkuya Salum, (kushoto) akijadiliana
jambo na Mbunge wa Peramiho,CCM, Jenista Mhagama, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Bunge walipokutana ndani ya ukumbi wa bunge, wakati wa
mjadala wa vipaumbele vya maendeleo ya Taifa, uliowasilishwa bungeni na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na uratibu Stephen Wasira.
Mbunge
wa Msalala CCM,Ezekiel Maige, akichangia mjadala wa vipaumbele vya
maendeleo ya Taifa uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais mahusiano na Uratibu,Stephen Wasira,Maige aliisisitiza Serikali
iangalie jinsi wananchi wasivyonufaika na rasirimali za Taifa lao
yakiwemo madini ya dhahabu kutoka kwenye migodi mikubwa iliyoko jimboni
kwake.
Naibu
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Chalres Kitwanga, (kushoto)
akijadiliana jambo na Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama (kulia)Jimbo la
Peramiho na William Ngeleja (nyuma kulia) wa Jimbo la Sengerema,
walipokutana ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma ambako bunge hilo
linakutana katika mkutano wake wa 13.
Waziri
wa Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samweli Sitta, (kulia)
akijadiliana jambo na Mbunge wa Nzega CCM, Dk,Hamis Kigwangallah,
walipokutana ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Ddodoma,ambako mkutano wa 13
wa bunge hilo unaendelea kujadili hoja mbali mbali za Serikali na zile
za wabunge,ikiwamo ya vipaumbele vya maendeleo ya Taifa na ile ya
mapungufu yaliyojitokeza wakati wa kutekelezaji wa zoezi la oparation ya
tokomeza ujangili inayoendelea nchini.
Waziri
Mkuu aliyejiuzulu, Mhe. Edward Lowasa,(kulia) akibadilshana mawazo na
Wabunge wa CHADEMA, Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo
(katikati) na Said Alfi, wa Mpanda mjini walipokutana nje ya ukumbi wa
bunge mjini Dodoma mara baada ya kuahirishwa kikao cha bunge
kilichojadili kwa kina na kuazimia kuundwa kwa kamati teule ya bunge ili
kufutilia ukiukwaji mkubwa wa sheria uliofanywa na waliosimamia na
kuendesha zoezi oparation tokomeza ujangili.
No comments:
Post a Comment