WAKATI wadau mbalimbali wa habari nchini wakipigania sheria ya uhuru na haki ya kupata habari na ile ya kudhibiti utendaji wa vyombo vya habari, serikali imewasilisha bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Sheria hiyo ya mwaka 1976 inalalamikiwa na wadau kwa kutoa mamlaka makubwa kwa waziri mwenye dhamana ya habari kufungia magazeti mbalimbali akijiridhisha yameandika uchochezi, chuki au taarifa zinazosababisha mtafaruku kwa jamii.Marekebisho hayo yanaonekana ‘kuvitia kitanzi’ vyombo vya habari na waandishi wa habari wanaodaiwa kuchapisha habari zenye uchochezi au uvunjifu wa amani.
Adhabu kwa vyombo vya habari na waandishi watakaobainika kutenda makosa hayo, itakuwa ni sh milioni tano au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, alisoma muswada huo jana bungeni alipokuwa akiwasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali.
Werema alisema marekebisho hayo yanalenga kutekeleza Azimio la Bunge lililotaka serikali ipitie sheria zilizopo ili kuona kama zinatosheleza kuzuia lugha au kauli za uchochezi.
Alibainisha kuwa baada ya kupitia, serikali imebaini kuwa adhabu ya faini kwa makosa ya kuchapisha habari za uchochezi au inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani ya sh 150,000 ni ndogo na sasa iwe sh milioni tano.
Alisema wamefikia hatua ya kupendekeza adhabu kubwa baada ya kulinganisha na madhara ya kosa husika kwa jamii. Werema pia alisema wamependekeza yafanyike marekebisho ili adhabu ya kosa la kutoa matamshi katika mikusanyiko ya watu yanayoweza kusababisha vurugu au kuchochea uadui baina ya makundi mbalimbali ya jamii iwe faini isiyopungua sh laki tano au kifungo kisichopungua mwaka mmoja.
Alibainisha kuwa kosa hilo kabla ya kupitishwa sheria hiyo, adhabu yake ilikuwa ni sh 1,000.
Pia maekebisho mengine yaliyofanyika ni kanuni ya adhabu kwa kosa la kutumia lugha ya matusi, kupigana na vitisho vya kufanya vurugu ambapo sasa adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja badala ya miezi sita iliyokuwapo awali.
Wapinzani wapinga Kupitia Tundu Lissu
Aliongeza kuwa vifungu hivyo viliingizwa katika sheria za Tanzania mwaka 1953 na vililenga kuwadhibiti wakosoaji na wapinzani wa sera na dola ya kikoloni waliokuwa wameanza kujitokeza katika miaka hiyo.
Alibainisha kuwa muathirika wa kwanza wa vifungu hivi alikuwa Baba wa Taifa, hayati Julius Nyerere, wakati huo akiwa rais wa chama cha siasa cha upinzani kiitwacho Tanganyika African National Union (TANU) na wenzake wawili. Walishitakiwa kwa kuchapisha kauli ya Mwalimu Nyerere kwamba wakuu wa wilaya wa kikoloni waliokuwa wanazuia mikutano ya hadhara ya TANU walikuwa wapumbavu. “Wakoloni walidai kwamba kauli hiyo ya Baba wa Taifa ilikuwa ya kichochezi na ya kashfa kwao, hivyo basi, wakoloni walimfungulia mashitaka ya jinai kwa kutumia kifungu hiki hiki ambacho leo, miaka 56 baadae, Bunge lako tukufu linaombwa kukirekebisha kwa kukiongezea adhabu,” alisema.
Alisema mwaka 1976 sheria ya magazeti ilianzishwa kwa lengo la kudhibiti na kuminya uhuru wa habari na haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari. Aliongeza kuwa mwaka huo huo sheria ya Shirika la Habari Tanzania (Shihata) iliyokuwa na lengo la kudhibiti ukusanyaji, upokeaji na utoaji habari ndani na nje ya Tanzania ilitungwa.
Lissu alisema sheria hiyo ilipiga marufuku ukusanyaji, upokeaji na utoaji habari ambao haukufanywa na Shihata au chini yake au kwa mamlaka yake kwa kuyafanya kuwa makosa ya jinai yenye adhabu ya faini na/au kifungo. Aliongeza kuwa sheria hiyo ilifutwa mwaka 2000, na Bunge lilitunga sheria nyingine ambayo ilitoa fursa kwa Idara ya Habari (Maelezo) kufanya kazi ya Shihata.
Alibainisha kuwa mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya magazeti hayana msingi kwa sababu hakuna ushahidi wa kuonyesha adhabu zilizoko zimeshindwa kudhibiti makosa ya uchochezi. Kwa mujibu wa Lissu, serikali imejenga utamaduni wa kufungia magazeti na kutisha waandishi wa habari, na imefikisha marekebisho hayo bungeni kwa malengo ya kisiasa ya kudhibiti wakosoaji na wapinzani wa serikali na watawala na sio kuzuia makosa ya jinai.
Lissu - Jukumu la mahakama kuadhibu si serikali
Tundu Lisu abainisha serikali kuingilia muhimili wa Mahakama kuhukumu
“Badala
ya kuwapeleka wakosaji wa aina hiyo mahakamani wakaadhibiwe kwa mujibu
wa sheria hiyo, serikali hii ya CCM imejenga utamaduni wa kufungia
magazeti na kutisha waandishi wa habari,” alisema. Lissu aliongeza kuwa
kwa kipindi chote hicho, serikali hii ya CCM imekataa kutekeleza
mapendekezo ya Tume ya Nyalali. Badala yake Tanzania imegeuka kuwa taifa
lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala.“Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa serikali hii ya CCM. “Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa wizara na serikali hii ya CCM kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua,” alisema Lissu.
Mbunge Akonay ataka serikali iachie madara vyombo husika
Naye
Mbunge Mbulu, Mustapha Akonay (CHADEMA), alisema kuwa kila taaluma ina
kanuni na maadili yake, hivyo akashauri kuwa badala ya serikali
kuwanyang’anya uhuru wanahabari na vyombo vya habari, kazi hiyo iachwe
kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Mbunge Mbarouk CUF adai marekebisho ni kuvikomoa vyombo vya habari
Rajab
Mbarouk wa CUF alipinga vikali adhabu hizo zinazopendekezwa, akidai ni
kutaka kuvikomoa vyombo vya habari jambo ambalo ni hatari sana.
CCM washangilia wakati Jenister akitaka sheria yote ipitiwe upya
Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (CCM), alisema anashangazwa na uamuzi wa serikali wa kuifanyia marekebisho sheria hiyo kila mara badala ya kupeleka muswada wa sheria ya kusimamia vyombo vya habari.
“Mnahofia nini? Si mlete muswada wa sheria ya magazeti ili tuiunde upya? Nina imani ikiletwa hapa itakuwa mkombozi mkubwa kwa tasnia ya habari,” alisema.
Pindi chana alalamikia baadhi ya magazeti kutumiwa na vikundi
Zambi hakuna kasoro yo yote ila asifia mswada
Mbunge
wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), alisifu hatua hiyo ya serikali
kuyabana magazeti, akidai wapinzani wanapinga kwa vile ndio wanayatumia
kutoa kauli za kichochezi.CHANZO JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment