Mtoto Neema enzi za uhai wake. |
Inauma
sana! Mtoto Neema Nyamuhanga mwenye umri wa miaka mitano, mkazi wa
Mlandizi, Pwani ameuawa kikatili na watu wasiojulikana kisha mwili wake
kutelekezwa porini.
Mwili
wa mtoto Neema uliokotwa na wachunga ng’ombe katika pori la Disunyara
lililopo kilometa saba kutoka nyumbani kwa akina Neema, Mlandizi Novemba
mosi, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwili huo ulikuwa umenyofolewa
koromeo, meno yote ya chini na sehemu za siri huku nguo ya ndani ikiwa
imewekwa pembeni.
Mama mzazi wa mtoto Neema (katikati) akilia kwa simanzi. |
Akizungumza
kwa masikitiko na gazeti hili, baba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa
jina moja la Nyamuhanga, alisema Novemba 27, mwaka huu, Neema alifika
nyumbani akitokea shuleni kwani alikuwa anasoma darasa la awali na
kutaka mama yake ampe chakula.
Baada ya kula, Neema aliondoka na hakurudi hadi usiku, jambo ambalo liliwashtua wazazi wake na majirani walioanza kumtafuta.
Mwili wa mtoto Neema. |
ALIJITABIRIA KIFO CHAKE?
Mtoto
Neema alijitabiria kifo chake kwani baada ya kula chakula alimwambia
mama yake kuwa amechoka na maisha anaondoka lakini mama yake alipuuzia
na kuona ni maneno ya kitoto.
Cha kushangaza kweli mtoto huyo aliondoka kama vile anaenda kucheza na hakurejea tena nyumbani.
Jeneza lenye mwili wa Neema likifunikwa. |
ATAFUTWA KWA SIKU SITA
Kwa
mujibu wa baba Neema, walijitahidi kutoa taarifa polisi, misikitini na
kumtafuta katika shule mbalimbali za Mlandizi ambapo watoto wachache
walikiri kumuona akipita mitaa yao lakini hakuna aliyejua wapi mtoto
huyo alipoelekea.
Kutokana
na kutafuta kila sehemu bila mafanikio kwa siku sita, walitafuta njia
nyingine ambapo walitumia waganga wa kienyeji kwa ajili ya kumrudisha
mwanaye.
...Jeneza likitolewa nje ya nyumba. |
“Kweli
inaniuma sana, nimepata maiti ya mwanangu, bado siamini maana nilikuwa
na huyu mtoto mmoja tu na miezi michache iliyopita mke wangu alikuwa
mjamzito mtoto akafia tumboni,” alisema mzazi huyo huku akifuta machozi.
USHIRIKINA WATAJWA
Katika
msiba huo, wengi walikiri kuwepo kwa ushirikina kutokana na jinsi mtoto
huyo alivyopotea, waganga walivyotoa vitu vya ajabu ndani ya nyumba
hiyo na mtoto kutolewa baadhi ya viungo.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Neema likiwa mbele ya waombolezaji. |
ALAZWA LUPANGO
Kutokana
na waganga hao kuwepo nyumbani kwake, kundi kubwa la watu lilijaa na
kusababisha polisi kufika eneo hilo na kumchukua baba Neema pamoja na
waganga watatu ambapo alilala lupango siku mbili katika Kituo cha Polisi
cha Mlandizi kwa kile kilichodaiwa kuwa hakuwa na kibali cha kujaza
watu nyumbani kwake.
Mwili wa mtoto Neema ukiombewa kabla ya mazishi. |
Baba Neema alisema uchunguzi wa daktari ulionesha kuwa mtoto wake aliuawa mbali na kutupwa eneo hilo.
Kutokana
na maiti hiyo kuharibika vibaya ilipelekwa moja kwa moja nyumbani kwao
na kuzikwa Novemba 2, mwaka huu katika makaburi yaliyopo maeneo hayo ya
Mlandizi.
Mama mzazi wa Neema akiwa na majonzi baada ya kuondokewa na mwanaye. |
Baadhi
ya majirani waliokuwa kwenye msiba huo walisema katika eneo lao hilo
kumekuwa na matukio mengi ya watoto kupotea katika mazingira ya
kutatanisha.
Mwili wa Neema ukizikwa. |
MWENYEKITI ANENA
Mwenyekiti
wa Mlandizi-Kati, Ali Bakari Nyambwili alikiri kutokea kwa matukio hayo
na kusema kuwa wamejiandaa kukomesha matukio hayo kwa kuanzisha ulinzi
shirikishi na utambuzi kwa kila mgeni atakayeingia katika kijiji hicho.
Waombolezaji wakiwa na huzuni. |
Mazishi yakiendelea. |
Kaburi la mtoto Neema.CHANZO GPL |
No comments:
Post a Comment