Mwanamke Aliyeuawa Kwa Kukatwa Kichwani Njombe.
Pichani
ni Anjelika Mhenga Aliyeuawa na Mtu Anayesadikika Kuwa ni Mumewe Jana
Majira ya Saa Tatu Asubuhi Mtaa wa Idundilanga Eneo la Ujamaa B Mjini
Njombe.
Mtuhumiwa
wa Mauaji ya Anjelika Mhenga Bwana Elia Mtweve Mkazi wa Kijiji cha Mkiu
Wilayani Ludewa Aliyetoroka Baada ya Kudaiwa Kumuua Mke Wake Njombe.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mtu Mmoja Mkazi wa
Matembwe Wilayani Njombe Anjelika Mhenga Mwenye Umri wa Miaka 37
Amekutwa Amefariki Dunia Baada ya Kupigwa na Kitu Chenye Ncha Kali
Sehemu za Kichwani na Mtu Anayesadikika Kuwa ni Mumewe Katika Eneo la
Ujamaa "B" Mtaa wa Idundilanga Mjini Njombe.
Akizungumza na
www.gabrielkilamlya.blogspot.com Kaka wa Marehemu Huyo Bwana Joseph
Mhenga Amesema Kuwa Tukio la Mauaji ya Dada Yake Limetokea Jana Novemba
26 Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu Asubuhi Baada ya Kupata Taarifa Kwa Njia
ya Simu na Mdogo Wake Ambaye Alieleza Kuwa Naye Kapigiwa Simu na
Shemeji Yake Kuwa Amegombana na Mkewe Hivyo Ameamua Kusafiri.
Aidha Bwana Mhenga Amesema Kuwa Shemeji Yake Huyo Anayedaiwa Kuhusika na
Mauaji Hayo Anafahamika Kwa Jina la Elia
Mtweve Mwenye Umri wa Miaka 41 Mkazi wa Kijiji cha Mkiu Wilayani Ludewa
Ambao Wote Kwa Pamoja Walikuwa Wakiishi Njobe Kama Mume na Mke.
Amesema Kuwa Hakuna
Taarifa Zozote za Sababu za Kutokea Kwa Tukio Hilo Walizozipata Zaidi ya
Taarifa za Ugomvi Waliokuwa Nao Licha Ya Kwamba Hata Ugomvi Huo
Haifahamiki Ulitokana na Nani.
Kwa Upande Wake Balozi wa
Eneo La Ujamaa 'B' Mtaa wa Idundilanga Bi.Catherine Nyatto Amesema Kuwa
Baada ya Kupata Taarifa za Tukio Hilo Akafika na Kubaini Tukio Hilo
Baada ya Kukuta Milango Yote Imefungwa Kwa Nje Ndipo Alipochukua Jukumu
la Kuvunja Mlango Mmoja wa Nje na Kisha Kwenda Kutoa Taarifa Polisi.
Hata Hivyo Mwili wa Marehemu Anjelika Mhenga Umeruhusiwa Kuzikwa Leo Huko Matembwe Tarafa ya Lupembe Ambako Ndiko Nyumbani Kwao.
CHANZO JACKSON AUDIFACE
No comments:
Post a Comment