Na Joseph Ngilisho, Arusha
HALI ya mwanamke aliyepigwa risasi na polisi katika Benki ya CRDB mjini hapa, Violet Lyapa (30) bado ni tete huku taarifa zake zikifanywa kuwa siri kubwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Selian, Violet bado
amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) huku hali yake
ikibadilikabadilika.
Pamoja na kwamba tukio hilo limechukua siku zaidi ya tano bado hali ya Violet inafanywa kuwa siri nzito.
Mwanamke huyo amewekewa ulinzi mkali katika wodi aliyolazwa lakini mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, amesema hali ya majeruhi huyo imekuwa ikibadilika kiasi cha kulazimika kumpa uangalizi maalum.
Jeshi la polisi mkoani hapa limekuwa na kigugumizi kutoa taarifa juu ya tukio hilo na hatua zipi zimechukuliwa juu ya uhalali wa umiliki wa silaha iliyotumia kuwatishia polisi baada ya kukuta gari lake limetolewa upepo.
Aidha, katika hali inayotia shaka kigogo wa ngazi za juu mkoani Arusha amekuwa akimjulia hali mara kwa mara majeruhi huyo hasa nyakati za usiku na taarifa zilizoenea zinasema kigogo huyo ana uhusiano wa karibu na majeruhi huyo.
Pia, baadhi ya ndugu wa majeruhi wamelalamikia kuzuiwa kumuona ndugu yao na kutakiwa kuonesha vitambulisho.
HALI ya mwanamke aliyepigwa risasi na polisi katika Benki ya CRDB mjini hapa, Violet Lyapa (30) bado ni tete huku taarifa zake zikifanywa kuwa siri kubwa.
Pamoja na kwamba tukio hilo limechukua siku zaidi ya tano bado hali ya Violet inafanywa kuwa siri nzito.
Mwanamke huyo amewekewa ulinzi mkali katika wodi aliyolazwa lakini mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, amesema hali ya majeruhi huyo imekuwa ikibadilika kiasi cha kulazimika kumpa uangalizi maalum.
Jeshi la polisi mkoani hapa limekuwa na kigugumizi kutoa taarifa juu ya tukio hilo na hatua zipi zimechukuliwa juu ya uhalali wa umiliki wa silaha iliyotumia kuwatishia polisi baada ya kukuta gari lake limetolewa upepo.
Aidha, katika hali inayotia shaka kigogo wa ngazi za juu mkoani Arusha amekuwa akimjulia hali mara kwa mara majeruhi huyo hasa nyakati za usiku na taarifa zilizoenea zinasema kigogo huyo ana uhusiano wa karibu na majeruhi huyo.
Pia, baadhi ya ndugu wa majeruhi wamelalamikia kuzuiwa kumuona ndugu yao na kutakiwa kuonesha vitambulisho.
No comments:
Post a Comment