Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM),Febronia Ikombe.
Mwenykiti wa
Chama Chama Mapinduzi (CCM) Kata ya Kahama Mjini wilayani hapa, Mkoa wa
Shinyanga, Febronia Ikombe, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa
kipigo na jamii ya wafugaji.Mwenyekiti
huyo anadaiwa kushambuliwa Jumanne iliyopita saa 5.00 asubuhi katika
Kijiji cha Kanegele wilayani Masumbwe mkoa wa Geita baada ya kundi la
ng’ombe kuingia kwenye shamba lake la mpunga na kuharibu mazao.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi nyumbani kwake baada ya kutoka hospitali
alikokuwa akitibiwa, Ikombe alisema siku ya tukio alipokea taarifa
kutoka kwa wakazi wa Kijiji cha Kanegele kwamba kuna ng’ombe wameingia
shambani kwake.
Ikombe
alisema aliondoka na kwenda shambani akiongozona na watoto wake watatu
na dereva wake. Walipofika walikuta ni kweli ng’ombe hao wakiwa
shambani. Alisema kutokana na hali hiyo aliwafuata wachungaji wa mifugo
hiyo na kuwahoji kwa nini wameingiza mifugo shambani mwake.
Alisema
hakupewa jibu, badaka yake mmoja wa wachungaji aliyejulikana kwa jina
moja la Mwanasabuni alipiga mayowe hali iliyomshangaza Ikombe.
“Mara
niliona kundi la wanakijiji wakija shambani hapo wakiwa na silaha za
jadi, fimbo, mapanga na marungu, nilishtuka sana, nikamuuliza
Mwanasabuni kwa nini amepiga mayowe, hakunijibu,” alisema.
Alidai wananchi hao baada ya kufika walimshambulia kwa kuwapiga yeye na watoto wake wakitumia fimbo ambapo waliwajeruhi.
“Nimepasuka
sehemu ya kushoto karibu na jicho, nilizinduka nikiwa hospitalini
ambako nilishonwa nyuzi sita. Mtu aliyenipiga namkumbuka ni mgeni wa
mwana kijiji cha Kanegele. Kwa kweli imenisikitisha sana,” alisema
mwenyekiti huyo.
No comments:
Post a Comment