Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na
visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA
AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima
akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi
kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4)
Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo
huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo
hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye
chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale
bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu
waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.
Lakini walioishia kidato cha
kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema
kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na
matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu
wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano
wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili
kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia,
Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni
rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi
ndio utakwepo kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a
brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he
is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao
waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je
kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini
na wakati huohuo tuko mafunzoni. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama
kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi. Haya ndio madhara ya AKILI
NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA
No comments:
Post a Comment