Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 12, 2013

MWILI WA MTUHUMIWA ALIYEFARIKI DUNI AKIWA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA WATAMBULIWA NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU.


 BABA MZAZI  WA MAREHEMU   KASSIM  MZEE SAID  ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60,AKIONGEA NA MWANDISHI KABLA YA KUUCHUKUA MWILI WA KASSIM

MWILI WA MARHEMU KASSIM KABLA YA KUANZA SAFARI YA KWENDA DSM
MOJA YA MAAFISA WA POLISI AKIANDIKA MAELEZO MAFUPI TOKA KWA MZAZI WA KASSIMU KABLA YA KUKABIDHIWA MWILI HUO NA JESHI LA POLISI
BABA MZAZI  WA MAREHEMU   KASSIM  MZEE SAID  ATHUMANI MBOYA MWENYE KOTI JEUSI AKIBEBA MWILI WA MWANAE HUKU AKISAIDIWA NA BAADHI YA WALIOFIKA KUMSAIDIA MZEE HUYO
SAFARI YA KUELEKEA DSM YAANZA
§  MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA  SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM  SAIDI MBOYA NDUGU ZAKE WAWILI AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID  ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA  MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM.

§  BAADA YA UTAMBUZI NDUGU HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA  ALIKUWA  ANAITWA KASSIM  SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.

§  AWALI MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.KASSIM  SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA AKIWA KATIKA TARATIBU ZA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

§  MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.

§   BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.

§  WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.

§  MWILI WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA,  PIPI HIZO ZINA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140.TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA MADAWA HAYO.

§  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI  KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU KAZI YA TAIFA.

Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Picha na Mbeya yetu
 

No comments:

Post a Comment