Pages

Friday, November 1, 2013

NAKO 2 NAKO WASEMA IBRA DA HUSTLER RUKSA KURUDI KUNDINI..


Inawezekana ile list ya zamani ya wanajeshi members wa kundi la Nako 2 Nako ikarudi tena hivi karibuni baada ya kumpunguza Ibra Da Hustler miaka kadhaa iliyopita.
Hii imethibitishwa na member wa Nako 2 Nako, G- Nako ambae ameiambia tovuti hii kuwa kuna uwezekano wa Da Hustler kurudi N2N japo bado hawajakaa kulizungumzia swala hilo, lakini cha msingi ni kwamba ‘it’s possible’.
“Yote yanawezekana..lakini sasa hivi bado hatujakaa kuzungumzia hilo swala.” Amesema Warawara.
Tulitaka kufahamu kama kweli 'hilo' linawezekana..au ni vile 'yote yanawezekana', “inawezekana ndiyo, inawezekana.” Alisisitiza ‘The Finest wa AR’.
Wiki mbili zilizopita Ibra Da Hustler’ aliuambia mtandao huu kuwa ana mpango wa kufanya project na wasanii wa kundi la Nako 2 Nako na kwamba hadi sasa wao ni kama familia na wanawasiliana mara kwa mara.
G- Warawara amethibitisha mpango wa kufanya project na Ibra Da Hustler.
“Project.. mi nilikuwa nataka kufanya nae lakini sasa mambo yaliingiliana, lakini kuna project tutafanya ndiyo, tutafanya lakini bado sijajua ni lini..ni wimbo wake ulikuwa, yeah wimbo wa Ibra.” Amesema G-Nako.
Kundi hilo kwa sasa linaundwa na Lord Eyez, G-Nako na Bou Nako.
Kwa maelezo zaidi, sikiliza The Jump Off ya 100.5 Times fm, leo usiku kuanzia saa mbili kamili hadi saa nne kamili usiku ambapo kila ijumaa inakuwa ni maalum kwa hip hop 'Hip Hop 100%', Jabir Saleh aka Kuvichaka ataiongoza show kama kawaida. Unaweza kusikiliza kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa 'Listen Live'.
Bofya hapa kumsikiliza G-Nako http://bit.ly/180YK0Y

No comments:

Post a Comment