Mkuu
wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono
na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati
walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu
wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es
Salaam. .Msanii
Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea mmoja wa wanafunzi wenye
ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam.
Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na
Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni
mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini
waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.
Wasanii
wa kundi la P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto
mwenye ulemavu wa Usonji, Erick wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda
kushiriki kutoa msaada kwa kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni
mwalimu mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na kulia ni Mkuu wa kitengo cha
Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine
wa kampuni hiyo.
Wasanii
wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye
ulemavu wa usonji wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam.
Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya
Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa
shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
Wasanii
Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule
wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji wa shule ya msingi ya
Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho
kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.
Waviomba
kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini · kufanya onesho kwa masaa
mawili mfululizo · Washiriki katika shughuli za kijamii Baada ya
kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye
maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa vyombo vya habari nchini
kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama
vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika
Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja
vya Leaders Club.
Wakizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hyatt
jijini Dar wasanii hao wamesema wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata
kutoka kwa jamii ya Watanzania na waandaaji wa Tamasha hilo na kuahidi
burudani ya kipekee kwa Watanzania. Peter Okoye ambaye ni mdogo wake na
Paul alisema, vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuwajenga
wasanii huku akitoa wito kwa vyombo hivyo kuwa kichocheo cha kuwajenga
wasanii na sio kuwabomoa.
“Vyombo
vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi kutujenga na
kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama vyombo vya hapa
nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa ndani nao waweze
kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku tukiwaona wasanii
kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi tulivyokuja nchini
kwao, alisema Paul.
Paul
Okoye ambaye ni kaka kwa Peter amesema “Tumefurahishwa sana na mapokezi
tuliyoyapata tangu jana usiku hadi kufikia sasa, tumejisikia faraja kuwa
katika nchi hii ya Tanzania watu wake ni wakarimu sana sifa hizi
tumezisikia kwa watu mbalimbali na tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi
Mashabiki wetu kufanya Shoo ya uhakika., alisema Paul Okoye. Kwa upande
wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema wamejisikia faraja kwa pamoja
kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania na
kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa
msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia mfuko
wa kusaidia jamii wa Vodacom”
Vodacom
Foundation”. “Kwa upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu kimekamilika
kuanzia, masuala ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika, Pamoja na
mambo mengine tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana onyesho
litaanza saa 1 na kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo hiyo na
kujiepusha na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa
amani. Wasanii kutoka Bongo watakao toa burudani katika Tamasha hilo ni
pamoja na wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo Makini”mwamba wa
kaskazini”pamoja na Ben Pol.
Wakati
huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom
Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto
wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini Dar es
Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuwasaidia
watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa kwa wote.
No comments:
Post a Comment