Rapcellency, da prezident na mfalme wa bling Prezzo wa 254 ameamua
kukata vilimilimi vya haters wake kwa kuamua kumuweka hadharani mlinzi
wake, bunduki ya AK 47, na kikubwa zaidi ni Gold Plated .
Prezzo amekuwa akizungumza na haters wake kwa vitendo, kwa kupost
Instagram picha mbalimbali zinazoonesha kuwa hana ‘njaa’ kama
walivyowahi kusema baadhi ya ‘maadui’ zake wakiwemo Huddah pamoja na
dada mwingine aitwaye Ashley Toto waliowahi kusema amepigika.
Katika picha ya bunduki Prezzo aliandika “Nobody lied…….. iam a star & got a chopper in the car #TrulyUnruly #Rapcellency”
Katika picha nyingine shemeji yetu Prezzo ameonesha saa yake ya Rolex pamoja na pete vyote vikiwa ni Gold.
“I know u want the finer things in life & I can get em 4 u, all u have to do is decide how bad u want em’ #Rolex KissThePinkyRing #Rapcellency #TrulyUnruly” aliandika Prezzo katika picha hii
Source: Bongo5
No comments:
Post a Comment