Watu
wawili wamefariki dunia papo hapo wilayani Bukombe mkoani Geita
wakitumia usafiri wa bodaboda kufuatia pikipiki waliyokuwa wakisafiria
kuteleza kwenye mchanga ikiwa kwenye mwendo kasi na kisha kukanyagwa
vibaya vichwani na gari aina ya Noah ambayo walikuwa wakipishana nayo.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, dereva wa bodaboda ambaye alikuwa na
abiria wake mwanamke mwenye mizigo, alikuwa katika mwendo wa kasi.
Hatua
kadhaa kabla ya kupishana na gari hilo, matairi ya pikipiki yake
yalishindwa kuhimili mchanga uliopo barabarani ndipo alipokosa uwiano wa
kumiliki chombo hicho cha usafiri na kutereza kisha wakaanguka katikati
ya barabara.
Sekunde
chache gari la abiria aina ya Noah ambalo mpaka shuhuda huyo anaondoka
kwenye tukio la ajali hakufanikiwa kulinasa namba zake likiwa kwenye
kasi liliwapitia vichwani bodaboda na abiria wake ambao walikufa papo
hapo.
-Gsengo
.
No comments:
Post a Comment