Pages

Wednesday, November 27, 2013

Picha na maelezo ya jinsi kivuko cha Dar – Bagamoyo kitakavyokua.


kivukoNakumbuka Waziri wa ujenzi John Magufuli aliwahi kusema moja kati ya mbinu kubwa za kurahisisha miundombinu na kupunguza foleni kwenye jiji linaloongoza kwa kuwa na magari mengi Tanzania (Dar es salaam) ni kuanzisha kivuko ambacho kitakua na safari kati ya Dar na Bagamoyo.

Ni miongoni mwa mipango ambayo itatekelezwa ili kupunguza foleni lakini pia kurahisisha usafiri pamoja na kupunguza idadi ya ajali za barabarani ambazo zimekua zikitokea kutokana na uzembe wa Wamiliki na Madereva wa mabasi ya abiria.

No comments:

Post a Comment