Rais
Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mara moja mpango mkubwa wa ujenzi wa
kimataifa wa reli ya kati baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa ya
ujenzi wa miundo mbinu ya barabara kwa kiwango cha lami nchini kote.
Mh rais kikwete
ametangaza mpango huo mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
kimataifa,wakati akihutumia maelfu ya wananchi wa mji wa Old Maswa
wilayani Bariadi mkoani Simiyu muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi
kwa ujenzi wa barabara ya kilometa 71.7 inayojengwa na kampuni ya cc
ya nchini China kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni
70.
Hata hivyo rais
Kikwete,amesema serikali,imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa
miundombinu ya barabara yakiwemo madaraja ili kuchochea kasi ya ukuaji
wa uchumi, huku akisema kati ya madaraja makubwa matano yalipangwa
kujengwa baada ya uhuru,rais wa kwanza Mwl Julius Nyerere ameweza
kujenga daraja la Kirumi mkoani Mara na rais wa awamu ya tatu Benjamin
Mkapa amejenga daraja la mto Rufiji na sasa serikali yake imekamilisha
ujenzi wa madaraja matatu yaliosalia.
No comments:
Post a Comment