Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,Joseph Kabila, anatembelea eneo la
mashariki mwa Congo ambalo awali lilidhibitiwa na kikundi cha waasi wa
M23, ambacho kilishindwa katika mapigano dhidi ya majeshi ya Congo
yakisaidiwa na yale ya Umoja wa Mataifa, mwezi mmoja uliopita.
Anatarajiwa kuwasili eneo la Rutshuru -- eneo ambalo lilikuwa ngome kuu ya waasi karibu na mpaka wa Uganda.
Bwana
Kabila amefanya safari ya urefu wa kilomita mia tisa kwa njia ya gari
mashariki mwa Congo kuonyesha imani yake kuhusu kuimarika kwa usalama
katika eneo hilo.
Amevitaka
vikundi vingine vyenye silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
kujisalimisha, la sivyo vitashughulikiwa kama ilivyotokea kwa kikundi
cha M23.
Eneo la
Rutshuru lilikuwa chini ya udhibiti wa M23 kwa zaidi ya mwaka mmoja na
wakaazi wa eneo hilo wameiambia BBC kuwa waasi hao waliwaua na kuwateka
watu wengi.
No comments:
Post a Comment