Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 29, 2013

rekodi za dunia, hawa jamaa wanaizunguka dunia na hii Bajaji.. kumbe walikuja mpaka Tanzania



Bajaji 1Watanzania wengi tunafahamu Bajaji ni usafiri wa hapa na pale tu, yani sio usafiri wa kubeba abiria kwenye masafa marefu lakini Walimu wawili raia wa Uingereza wamekipiga kibajaji gia na kupita nacho nchi mbalimbali duniani zinazofikia 37.
Ni safari ambayo wameianza August 13 mwaka jana (2012) lakini haijafikia hapa bila matatizo, wanakwambia Bajaji imezingua sana kwenye baadhi ya nchi na kuna wakati injini ilisumbua wakajua ndio mwisho wa safari mpaka wakati mwingine wanalazimika kushuka na kuanza kuivuta wao wenyewe.
Unaambiwa hii rekodi itaingia kwenye kitabu cha Guiness kama watamaliza safari yao ambayo wamepanga kuimalizia Brazil kabla ya December 23 2013 kisha kurudi zao nyumbani Uingereza.
Wanasema wengine wameshindwa kuamini kama wanaizunguka dunia kwa ‘tuktuk’ a.k.a Bajaji ambapo kwenye mpaka wa Kenya na Uganda walisimamishwa na Polisi ambae aliwaambia haamini kuhusu urefu wa safari yao ila kama ni kweli, itakua ngumu wao kupata watoto wa kiume.. labda wa kike.
bajaj 3
bajaj 10Wakiwa South Africa.
bajaji 4Wakiwa Paris.
bajaji 5Wakielekea kwenye mpaka wa Hispania.
bajaji 6Barcelona Hispania.
bajaji 7
bajaji 8Wakizungumza na Wanafunzi Ethiopia.
bajaji 9Hapa kwenye picha ya juu ni Burundi.
bajaji 10Hapa kwenye vumbi, wameandika ni Magharibi mwa Tanzania.
bajaji 11Ni safari ambayo haijakwenda bila kasoro, hapa ni Northern Peru
.
 TUNAOMBA CLICK IYO LINK NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA UPDATES TOFAUTI TOFAUT

No comments:

Post a Comment