Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 1, 2013

SAKATA LA MWANAMKE KUPIGWA RISASI ARUSHA MAPYA YAIBUKA



 Gari lenye namba za usajili  T888 BWW aina ya Cresta  mali ya  Vaileth Mathias,likiwa chini ya ulinzi wa polisi,baada ya  Mathias  kupigwa risasi 
Toka jana jioni wakazi wa jiji la Arusha

wameendelea kuwa katika taharuki na minong'ono hapa na pale kutokana na
tukio la kupigwa risasi binti mmoja aitwaye Violeth Mathias katika 
ofisi za TRA Arusha.
Mwanadada huyu aliyeonesha jeuri ambayo 
haikutegemea si tu Arusha bali katika Taifa hili hasa lile la kwenda na 
kuchukua Bastola na kutaka kummaliza askari aliyekuwa akitimiza wajibu 
wake katika Bank ya CRDB. Kitendo hiki kimefanya wakazi wa jiji hili 
kuwa na Maswali mengi kuliko majibu. Hasa juu ya anakotoa jeuri ama 
kiburi mwanadada huyu.

Viola alikwenda CRDB kuchukua pesa na 

kilichotokea yeye alipaki gari eneo lisiloruhusiwa kwa mazingira yale ya
Bank. Hivyo askari Polisi alimfuata na kumwelekeza kwamba haruhusiwi 
kupaki gari eneo hilo ila yeye (Mwanadada) huyu hakutaka kusikiliza 
alichokuwa akiambiwa. Akashuka na kwenda bank ndani.

Hata hivyo Polisi alimfuata ndani ila 

cha kushanga mwanamke huyu akagoma tena. Ndipo Polisi kwa ajili ya 
usalama alirudi nje na kutoa upepo matairi yote ya gari kwa tahadhari. 
Cha kustaajabisha ni pale binti huyo aliporudi na kukuta hali hiyo 
alipoulizwa alijibiwa polisi ndiye aliyefanya hivyo. Alichofanya alienda
kwenye gari lake na kutoka na bastola ati akitaka kumlenga yule askari 
polisi ndipo yule askari alipoaamu kujihami na kumshut begani.
Baada ya watu kuchunguza wakajua kuwa 

kiburi hicho anakitia kwa RC wa Arusha Bwa. Magesa Mulongo kwa kuwa 
anajipumzisha kwake. Wakazi wengi wa hapa wameshangazwa sana namna RC 
anavyozidi kuchafua nafasi yake hiyo na hata yule aliyempatia.
Cha kusikitisha zaidi ni RPC kuamua 

kukimbia waandishi wa habari baada ya waandishi kumfuata na kumtaka atoe
maelezo juu ya hilo tukio. RPC kuona waandishi wa habari alimwamuru 
dereva kugeuza gari na kuondoka jambo lililopelekea waandishi wa habari 
kuamini kuwa RPC atakuwa amepokea maeleekezo toka kwa RC. 
RPC alipopigiwa simu aliishia kusema 

anaelekea Hospitali kwa kuwa Sukari yake haiko sawa hili limepelekea 
kuaminika kuwa Mulongo anawaweka viongozi wenzie katika wakati mgumu

 

No comments:

Post a Comment