Pages

Wednesday, November 6, 2013

SIMBA YAZINDUKA YAICHAPA ASHANTI GOLI 4 KWA 2


DSC_1027Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc, leo hii wamefufuka baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Ashanti United katika mchezo wao wa kufunga pazia la mzunguko wa kwanza ligi kuu soka Tanzania bara.Mabao ya Simba yamefungwa na Ramadhan Singano `Messi` , Betram Mwombeki aliyefunga mawili na Amissi Tambwe.Ashanti wao wamejipatia mabao yao kupitia kwa Hussein Swedi na Mkongwe Said Maulid `SMG`.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, hadi mapumziko tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1.
Timu hizo zilishambuliana kwa zam ambapo  Ashanti walipiga pasi nzuri na fupifupi wakati Simba wao walikuwa wanapiga mipira mirefu.

Licha ya ushindi huo, Simba sc wanabakia katika nafasi ya nne wakiwa na pointi zao 24, huku Yanga wakiwa nafasi ya tatu na pointi 25, Mbeya City na Azam fc wapo juu kwa pointi 26 na timu zote kesho zinacheza  mechi za kukamilisha ratiba ya mzunguko wa kwanza.
Mchezo mwingine umepigwa katika dimba la Azam Complex ambapo JKT Ruvu walikuwa wanakabiliana na Coastal Union na maafande hao kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ruvu Shooting walikuwa na kibarua mbele ya Mtibwa Sugar katika uwanja wao wa Mabatini na kushuhudia timu hizo zikichoshana kwa sare ya bao 2-2.
Kagera Sugar wamekamilisha ligi kuu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo Jkt katika dimba la Kaitaba.
Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara utamalizika kesho kwa mechi Tatu kupigwa viwanja vitatu tofauti.
Yanga watakuwa uwanja wa Taifa kuwakabili JKT Oljoro, Azam fc watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wao wa Azam Complex, nao Maafande wa Rhino Rangers watakuwa nyumbani Ali Hassan Mwinyi kuwakabili Tanzania Prisons.

No comments:

Post a Comment