Waziri wa
Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Mh. Said Ali Mbaruk akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)
kuhusu michezo mbalimbali itakayofanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayo adhimishwa Mwezi January
2014,wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
Leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO)
Frank Mvungi - Maelezo
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeandaa mashindano ya michezo 17
kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi hayo itakayofikia kilele januari
12,2014 ambayo ni siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari , Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar Mh.
Said Ali mbaruk wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya michezo ya
kuadhimisha mapinduzi hayo.
Mh. Said
Ali Mbaruk amesema kuwa katika kuadhimisha mapinduzi hayo michezo
mbalimbali itafanyika ikiwemo mpira wa miguu,riadha,volleyball,Table
tenis na mazoezi ya viungo.
Akifafanua
zaidi Alisema michezo hiyo pia itawahusisha watu wenye ulemavu ambapo
kwa kushirikiana na Kamisheni ya utalii michezo mingine itakayofanyika
ni karata,bao,squash na kuogelea .
Akieleza
zaidi Mh. Said Ali Mbaruk aisema kuwa katika michezo hiyo kutakuwa na
timu zaZanziba,Tanzania bara,Afrika Mashariki,ambapo mashindano hayo
yanapata hadhi ya kimataifa.
Pia
alizitaja timu zinazotarajiwa kushiriki kuwa ni Azam FC,Simba,
Yanga,Mbeya city kwa upande wa Tanzania bara, baadhi ya timu toka
Zanzibar ni chuoni,Pemba combine na Unguja combine.
Katika maadhimisho hayo mechi zote zitatangazwa moja kwa moja kupitia ZBC TV,kwa kushirikiana na Azam TV.
No comments:
Post a Comment