Pages

Tuesday, November 26, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


RPC  MBEYA
“PRESS RELEASE” TAREHE 26.11. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA
                                      KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 25.11.2013 MAJIRA YA SAA 12:45HRS HUKO MAENEO YA MADUGU, KATA YA ISANGATI, TARAFA YA  ISANGATI  BARABARA YA  MBALIZI/UMALILA WILAYA YA  MBEYA  MKOA WA MBEYA, GARI  T. 966 BKR AINA YA  MITSUBISH CANTER LIKIENDESHWA NA DEREVA  LUTIMO S/O SIMFUKWE, MIAKA 39, MNYIHA, MKAZI WA MBALIZI  LILIACHA NJIA KISHA KUPINDUKA NA KUSABABAISHA KIFO KWA YOHANA S/O SOLOMONI, MIAKA 28, MNYAKYUSA, FUNDI MAGARI MKAZI WA DDC MBALIZI NA MAJERAHA KWA ABIRIA 11. MAJERUHI WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI MBEYA KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI UTELEZI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ILI KUEPUKA AJALI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 26.11.2013 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO MTAA WA ILEMBO AIR PORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, PELIS D/O FREDRICK, MIAKA 35, MKINGA, MFANYABIASHARA SPAIR ZA PIKIPIKI MBALIZI NA MKAZI WA ILEMBO AIR PORT ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU KINACHODHANIWA KUWA KISU SEHEMU YA UBAVU WA KULIA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA AKIWA NYUMBANI KWAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA UKIWA NA MAJERAHA MANNE SEHEMU ZA UBAVU WAKE WA KULIA, HAKUNA KITU CHOCHOTE KILICHOCHUKULIWA NYUMBANI KWA MAREHEMU. CHANZO KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA MMOJA AMEKAMATWA KUTOKANA NA TUKIO HILI DANIEL S/O TWEVE, MIAKA 21, MKINGA, MFANYAKAZI WA DUKA LA SPAIR LA MAREHEMU MBALIZI NA MKAZI WA TUNDUMA ROAD. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment