Juma
Kaseja akisaini mkataba wa kuichezea Yanga mbele ya mjumbe wa kamati ya
utendaji ya Yanga Bin Kleb, nyuma Abdulfatah. Kaseja amesaini mkataba
wa miaka miwili kuitumikia Yanga.
|
Mlinda
mlango nambari moja nchini Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka 10
mfululizo Juma Kaseja Juma jana majira ya saa 2 usiku alisaini mkataba
wa kuitumikia klabu ya Young Africans yenye makao yake Twiga/Jangwani
kwa kipindi cha miaka miwili.
Usajili wa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya Yanga unafuatia
mapendekezo ya benchi la ufundi katika ripoti waliyoikabidhi kwa kamati
ya mashindano kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa ajili
mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.
Benchi
la ufundi chini ya kocha mkuu Ernie Brandts lilihitaji mlinda mlango
mwenye uzoefu wa michezo ya kimataifa kwa ajili ya kujiandaa na michezo
ya kimataifa na mzunguko wa pili ambao utakua na upinzani kulingana na
kila timu kutaka kufanya vizuri.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara
baada ya kumalizika kwa zoezi hilo mwenyekiti wa kamati ya usajili wa
klabu ya Yanga Abdallah BinKleb alisema hawana shaka na uwezo wa Kaseja
kwani rekodi yake ndani na nje ya nchi inafahamika kwa hiyo wanaamini
atatoa mchango mkubwa wa timu ya Yanga.
Timu yetu imekamilika kila idara, kikubwa tunachokifanya ni
kuhakikisha tunazidi kukiboresha na kuyafanyia kazi mapendekezo ya
benchi la ufundi ili kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri na
kutisha katika Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
"Najua wegine watajiuliza maswali mengi kwa nini Yanga wamemsajili
Kaseja, ukweli ni kwamba walinda mlango waliopo ndani ya Tanzania Kaseja
bado ana uwezo nkubwa na msaada ambao atautoa katika kukiimarisha
kikosi chetu" alisema Bin Kleb
Kaseja hakua na timu yoyote aliyoichezea katika mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na timu yake ya zamani ya
Simba SC hivyo kujiunga na Yanga kama mchezaji huru katika kipindi
hichi cha drisha dogo la usajili.
Kutua kwa Kaseja kunaifanya Yanga kuwa na walinda mlango wanne wote
wenye uwezo wa hali ya juu na kutokuwa na shaka wakati wowote timu
inapokuwa inakabaliana na mashindao yoyote iwe ni ndani ya nchi au ya
nje ya nchi (kimataifa).
Kaseja anaungana na walinda mlango wengine Ally Mustapha 'Barthez',
Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul ambao wataitumikia klabu ya
Yanga kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom januari 2014 na
mashindano ya klabu Bingwa Afika 2014.
No comments:
Post a Comment