Pages

Tuesday, November 5, 2013

TAZAMA PICHA:::MATAPELI WALIZA WATU TOFAUTI MWANZA ZAIDI YA MILIONI 309


Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Joseph Konyo  ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai akitoa taarifa.
WATU sita wametapeliwa kwa matukio tofauti,akiwemo mmoja aliyenunua kilo 10 za unga wa sembe kwa thamani ya shilingi Milioni 70 akidhani ni madini ya Rubi (Green Tourmaline) na mwingine kutoa shilingi milioni 200 akitaka zizalishwe ajipatie milioni 400 baada ya kudanganya na watu hao ambao ni matapeli mkoani Mwanza.


Matukio hayo ambayo niya kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu kutokana na wizi huo uliofanywa na makundi ya watu mbalimbali yanaujihusisha na utapeli, wananchi hao ambao baadhi ni watu maarufu Jijini hapa, ‘wamelizwa’  kiasi cha shilingi Milioni 309 kwa kipindi hicho.
 Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Joseph Konyo  ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoani hapa akitoa taarifa za matukio hayo jana kwa waandishi wa habari ofisini kwake, alisema kuwa ,baadhi ya matapeli waliokamatwa wameisha fikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea kusakwa. 
Katika tukio la hivi karibuni mwezi uliopita, mwananchi mmoja maarufu jijini Mwanza (hakutajwa) mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, alinaswa na mtego wa matapeli hao na kujikuta akiuziwa kilo kumi za unga wa sembe ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye begi ikidaiwa ni madini ya Rubi (Green Tourmaline)

“Huyu alilazimika kuuza nyumba yake jijini Mwanza na kwenda na matapeli hao hadi Morogoro ambapo alionyeshwa madini hayo na kutoa pesa na kisha kufungiwa kwenye begi bila kutakiwa kulifungua hadi atakapofika Mwanza na kukaa siku saba vinginevyo atakiuka masharti na kukuta majini.” Alielza Konyo.

Alieleza kuwa , baada ya siku tatu kupita, mkazi huyo aliwapigia simu wauzaji akitaka kufungua lakini walimzuia kuwa asubiri hadi watakapomueleza, akilazimisha atakuta majini, hali iliyomfanya akimbilie polisi ili kuomba msaada wa kulifungua na ndipo ilipobainika kulikuwa na unga wa sembe na si madini.

“Huwezi kuamini na ukimuona huto amini kama angesitahili kuibiwa kiurahisi (Kutapeliwa) namuna huyo ni mtu anaheshimika hata kimuonekano wake na kibaya zaidi alimpa talaka kwanza mkewe ndiyo akuza nyumba yake ili kupata fedha za kupata madini hayo, sasa mke kamkosa, nyumba imeenda, fedha na madini kavikosa.” Alisema. 
Tukio jingine, ni mkulima mmoja aliuza nyumba yake kwa thamani ya sh milioni 7 na fedha hizo kuuziwa chupa ya dawa feki ya kuhifadhia mazao ambayo alidanyanywa kuwa angeweza kuiuza kwa wakulima wenzake kwa sh milioni 100 na kwamba dawa hiyo inatafutwa na wazungu na inapatikana katika Chuo cha Utafiti Ukiriguru pekee hivyo kwake atweza kuvuna kiasi hicho.       

“Mwingine aliuziwa chupa tatu za chuma (Mitungi midogo) zilizojazwa kokoto na cimenti (ndani) kwa tahamani ya shilingi milioni 26, akidanganywa kuwa ni za asidi (mercury)  ya kuoshea  dhahabu na mwingine akadanganywa asiweke fedha benki wamuuzie dhahabu, akauziwa gorori za baiskeli kwa shilingi milioni 6 baada ya kuonyeshwa vipande vya kufuli vilivyosagwa na kung’aa kama dhahabu.” Alisema Konyo. 
Kamanda huyo alieleza kuwa, katika tukio jingine, mwananchi mmoja aliyeuza nyumba yake shilingi milioni 200, alidanganywa kuwa wanaweza kuzarisha fedha zake mara mbili na kuziweka kwenye boksi la mganga mmoja ili ziwe sh milioni 400, matokeo yake alibiwa, watuhumiwa walikamatwa kesi iko mahakamani.

Akihitimisha matukio hayo la mwisho, alisema kuwa mwanamke mmoja mfanyabiashara alijikuta akibakwa, kulawitiwa na kuibwa pesa (hazikutajwa) baada ya kufanya mazungumzo katika chumba cha Hoteli moja jijini hapa na kujikuta akinyweshwa dawa za kulevya na watu hao waliojitambulisha kwake kuwa ni wafanyabiashara kutoka Miji mikubwa

Kaimu kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza, alisema matapeli hao wakati mwingine wanatumia majina ya viongozi wa ngazi za juu mkoa na taifa hivyo wawe makini kubaini mbinu zinazotumiwa na ikiwezekana kutoa taarifa mapema kabla ya kutoa fedha kwani mbinu nyingine ni za kizamani, zinahitaji akili ya utambuzi wa ukweli na uongo.

“Ebu sasa viongozi na wafanyabiashara ambao kila kukicha matapeli wanapanga njama za kuwadanganya kwa lengo la kuwaibia na kuwatapeli wafanye mawasiliano kwanza emdapo matapeli hao watawafika na kutumia majina ya viongozi wengine wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya kutekeleza kile walichoombwa ikiwemo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kuwakamata” alisisitiza
 
KWA HISANI YA G SENGO BLOG

No comments:

Post a Comment