KATIKA hali ya kushangaza, mwanaume mmoja, Maige Masyome (29) amechomwa
kisu na mwenzake, Amosi Anthony kwa kosa la kukataa kumnunulia pombe ya
kienyeji, tukio lililotokea Novemba 10, mwaka huu, Kigonga, Nyamunge
mkoani Mwanza.
Alidai
Amosi alibadilika na kuanza kumlazimisha na alipozidi kukataa alinyamaza
lakini wakati akiinuka kuondoka zake eneo hilo, Amosi alimchoma kisu
shingoni.
“Nilishangaa
baada ya kuona anazidi kunizonga nimnunulie pombe, nilipokataa akakaa
kimya. Sasa wakati nainuka nilishangaa jamaa anasimama na kunichoma kisu
shingoni,” alisema Maige kwa taabu.
Kwa
upande wake, kaka wa mgonjwa huyo aitwaye Wambura, alisema walifungua
kesi katika Kituo cha Polisi cha Nyamango kwa jalada NYM/RB/3291/2013 na
kuongeza kuwa wamepata taarifa kuwa mtuhumiwa bado yupo uraiani
akitembea bila wasiwasi wakati ndugu yao anateseka hospitali.
“Nimepata
taarifa kuwa mtuhumiwa anatembea bila wasiwasi mtaani wakati mdogo
wangu anateseka hapa ndani. Ninaomba mtuhumiwa akamatwe ili sheria
ichukue mkondo wake,” alisema Wambura.
Hadi sasa
Maige amelazwa katika Hospitali ya Bugando akiendelea na matibabu huku
akiwa amepooza sehemu ya mwili wake kuanzia kifuani hadi miguuni.
No comments:
Post a Comment