Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda
kesho tarehe 29, Novemba 2013 anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Uzinduzi wa Tovuti Kuu hiyo inayopatikana kwa anuani ya www.tanzania.go.tzutahudhuriwa
na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wananchi, Wafanyabiashara,
Washirika wa Maendeleo, Taasisi zisizo za Serikali na Wawakilishi kutoka
vyuo Vikuu.
Tovuti
Kuu hiyo ni mojawapo ya juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa
taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia
wananchi kwa urahisi, wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya
nchi. Tovuti Kuu hiyo pia ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza
dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma
zinazotolewa na Taasisi za Serikali kwa urahisi.
Taarifa
na huduma katika Tovuti Kuu hiyozimegawanywa katika maeneo makuu sita
ya ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya
Nje inalenga kutoa huduma mbalimbali kama upatikanaji wa nyaraka zote
za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na
mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.
Huduma
nyingine katika Tovuti Kuu hiyo imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje?
ambao unamjengea uwezo mwananchi wa kufahamu taratibu za upatikanaji wa
huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama nifanyeje
kupata pasipoti, kibali cha kazi, TIN, Cheti cha kuzaliwa na mikopo ya
chuo.
Aidha
tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi
mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara
katika dirisha moja.
Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz
chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Tovuti hiyo
iliboreshwa na kuunganishwa na iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
No comments:
Post a Comment