Pages

Wednesday, November 13, 2013

Viwanja sita vyafungwa Ligi Kuu



Dar es Salaam. Bodi ya Ligi (TPL) imefunga viwanja saba vilivyokuwa vikitumika katika mzunguko wa kwanza Ligi Kuu na  Ligi Daraja la Kwanza kutokana na uchakavu na havifai kutumika kwa mashindano.
Hatua hiyo imefikiwa na bodi hiyo Jumapili iliyopita baada ya kukutana kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake ili kupitia ripoti mbalimbali zilizokuwa zikihusiana na mzunguko wa kwanza wa ligi hizo uliofika tamati hivi karibuni.
Viwanja vilivyofungiwa ni Ali Hassan Mwinyi wa Tabora, Mkwakwani (Tanga), Kaitaba (Bukoba), Jamhuri (Morogoro), Sokoine (Mbeya), Majimaji (Songea) na Sheikh Amri Abeid (Arusha).
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),  Boniface Wambura alisema kuwa viwanja vya Ali Hassan Mwinyi na Mkwakwani vimefungiwa kutokana na vyumba vya kubadilisha nguo kuwa ni vibovu.
Alisema vyumba vya Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi pia vimekuwa vikitumika kama shule ya chekechea wakati Uwanja wa Kaitaba majukwaa yake ni mabaovu na yatishia usalama wa watu wanaofika uwanjani hapo.
“Hata hivyo viwanja vya Jamhuri Morogoro, Sokoine, Majimaji  na Sheikh Amri Abeid ubovu wake ni katika sehemu ya kuchezea.
“Kutokana na hali hiyo kamati imeagiza vifanyiwe ukarabati, hivyo timu husika ambazo zinavitumia kwa ajili ya mechi zake inabidi ziwasiliane na wamiliki wa viwanja hivyo kwa lengo la kufanyiwa ukarabati mapema iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hizo.
“Endapo mpaka kufikia muda huo kama itakuwa bado havijafanyiwa ukarabati huo basi timu hizo zitalazimika kutafuta viwanja vingine ambavyo vitakuwa vinakidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa ajili ya michuano hiyo,” alisema Wambura.
Katika hatua nyingine kamati hiyo imezitoza faini baadhi ya timu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza ikiwa ni pamoja na baadhi ya wachezaji na viongizi wako kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu kwenye muzunguko huo wa kwanza wa ligi hizo.
Timu ya Mbeya City imelimwa faini ya Sh 1.5 milioni kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu waliyofanya  viongozi na mashabiki wa timu hiyo.
Makosa hayo ni pamoja kutoingiza uwanjani kikosi chake cha vijana kucheza mechi ya utangulizi kabla ya mchezo wake wa LigiuKuu dhidi ya Coastal Union pia mashabiki wake kufanya vurugu wakati wa mechi yake dhidi ya Yanga na Prisons.
Hata hivyo mbali ya faini hiyo pia wametakiwa kulipa gharama za uharibifu uliotokana na fujo hizo ikiwa ni pamoja na kuvunja vioo vya basi la Yanga, gharama hizo zitalipwa baada ya kuthibitishwa na Kamati hiyo ya ligi.Timu nyingine zilizokumbana na rungu la kamati hiyo ni Cocastal Union ambayo ililimwa faini ya Sh 500,000 baada ya wachezaji wake kufanya fujo katika mechi yao dhidi ya Azam.chanzo mwanainchi

No comments:

Post a Comment