Ujenzi wa daraja Kigamboni. |
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limesema ujenzi wa daraja la
Kigamboni, upo katika hali nzuri, ingawa kuna changamoto ya wananchi
kumi ambao hawajahama, kupisha ujenzi huo.
Meneja
Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Eunice Chiume
alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi
wa habari.
"Ujenzi
wa daraja unaendelea vizuri sana, ila changamoto ni wale wanaotakiwa
kulipwa fidia kugoma kuondoka, kwa upande wa Kigamboni wapo watu wanane
na upande mwingine wapo wawili," alisema.
Aliomba
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati suala hilo ili
ujenzi uendelee kama ulivyopangwa na hatimaye daraja likabidhiwe ifikapo
2015.
Katika
hatua nyingine, NSSF imejenga nyumba 279 za bei nafuu katika eneo la
Kijichi wilaya ya Temeke, ambazo zitauzwa kwa wanachama wake kwa fedha
taslimu au mkopo.
Alisema
nyumba hizo ambazo awali zilikuwa zikiuzwa kwa mkopo kupitia Benki ya
CBA kwa sasa mkopo huo utatolewa na shirika hilo kwa riba ya asilimia
11.4 kwa mwaka kwa miaka 15.
Alisema
nyumba hizo zipo za aina tofauti kuanzia za vyumba viwili hadi vinne na
bei zake huanzia kati ya Sh 64,875,310 hadi Sh 112,500,000 bila VAT
kulingana na aina.
Alisema
wanachama ambao wangependa kuwa wanunuzi wa nyumba hizo wafike katika
ofisi za NSSF kwa ajili ya maelezo zaidi na huduma.
No comments:
Post a Comment