Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 5, 2013

WATU 6 MBARONI KWA KUMCHARANGA MAPANGA DKT MVUNGI



Kamanda Suleiman Kova akiongea na wanahabari kuhusu wahalifu mbalimbali waliotiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
Baadhi ya vitu walivyokutwa navyo wahalifu katika matukio mbalimbali jijini Dar es Salaam.
WATU 6 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio la kumshambulia Dkt. Sengondo Mvungi aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake Kibamba Msakuzi juziAkizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova amesema katika operesheni maalum iliyofanywa na jeshi la polisi, wamefanikiwa kuwakamata watu sita ambao majina yako yamehifadhiwa kwa sababu za usalama. Aidha Kamanda Kova aliongeeza kuwa bado hawajapata uthibitisho kamili juu ya sakata hilo na uchunguzi unaendelea kuwabaini wahusika halisi wa shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment