Pages

Monday, November 25, 2013

Watu 7 wafariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali Tanga.


 
 Watu saba wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa vibaya baada ya magari mawili ya abiria yanayofanya safari zake kutoka jijini Tanga kwenda wilayani Korogwe kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Chang'ombe kilichopo katika barabara kuu inayounganisha mikoa ya Tanga kwenda Kilimanjaro.
Waliofariki katika ajali hiyo wametambulika kuwa ni Ramadhani Waziri kondakta wa Concorde, Jumanne Abdalla dereva wa basi hilo dogo, Nuia Mohamed abiria,Shamina Mbago abiria,William Samwel abiria,Martin Msembo na mmoja ambaye hadi sasa mwili wake haujatambuliwa.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakizungumza na ITV katika hospitali teule ya wilaya ya Korogwe ya magunga ambapo wamelazwa kwa ajili ya matibabu wamesema madereva wa magari yote mawili ya kampuni ya mabasi ya ''Zamoyoni na concorde''walikuwa katika mwendo kasi hivyo wakati wakiwa katika harakati za kukwepa mbuzi huku wengine wakidai kuwa ni mbwa na mwanae waliokuwa wakivuka barabara ndipo walipogongana uso kwa uso na kusababisha watu watano kufa papo hapo.
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Korogwe Dr. Rashid Said amesema katika ajali hiyo wamepokea majeruhi 24 na miili mitano ya waliofariki isipokuwa baadae katika majeruhi wanne waliokuwa na majeraha makubwa sehemu za kichwani wawili kati yao walifariki na kuongeza idadi kufikia saba.
Naye kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga Costantine massawe ametoa wito kwa madereva kuheshimu maisha ya abiria badala ya kukwepa mbuzi hivyo amewataka wakazi wanaofuga mifugo yao pembeni mwa barabara kufungia mifugo ili isiweze kusababisha ajali barabarani.



No comments:

Post a Comment