MBUNGE wa
Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye Chadema imemvua wadhifa
wa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kwa maelezo kuwa anakihujumu,
amefurahia ulaji mpya aliopewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. Malinzi
amemteua Zitto kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ya
TFF kwenye kamati mpya zilizotangazwa juzi, Jumamosi.Zitto alitamka jana
Jumatatu kuwa: "Nashukuru nasikia Malinzi ameniteua Kamati ya Fedha ya
TFF, labda ndiyo kazi nyingine ninayokwenda kufanya huko."Zitto ambaye
ni shabiki wa Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England pamoja na Simba
yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Dar es Salaam alisema: "Mimi nina
wakati mgumu maana wakati wenzetu Yanga wanapanga mikakati ya ushindi
Simba wanapigana na kupinduana, jana nilitarajia Liverpool watatupa
ahueni kidogo lakini wametoka sare."
Alitoa kauli
hiyo
kutokana na mgogoro uliopo Simba kati ya kamati ya utendaji na
Mwenyekiti, Ismail Aden Rage na kuhusu Liverpool iliyoambulia sare ya
3-3 na Everton.
Zitto pia
alisisitiza azma yake ya kutojitoa Chadema katika mkutano ambao pia
ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, wengi
wakiwa ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma kama ilivyo kwa Zitto.
Wasanii
hao walichukua jukumu la kuwakaribisha waandishi wa habari katika
mkutano huo ni pamoja na Afande Sele', Peter Msechu, Mwasiti, Queen
Darlin na Baba Levo. Chanzo: Mwananspoti
No comments:
Post a Comment