Pages

Tuesday, November 26, 2013

ZITTO AFURAHIA ULAJI TFF


zitto1 f1a88
MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye Chadema imemvua wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kwa maelezo kuwa anakihujumu, amefurahia ulaji mpya aliopewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. Malinzi amemteua Zitto kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ya TFF kwenye kamati mpya zilizotangazwa juzi, Jumamosi.Zitto alitamka jana Jumatatu kuwa: "Nashukuru nasikia Malinzi ameniteua Kamati ya Fedha ya TFF, labda ndiyo kazi nyingine ninayokwenda kufanya huko."Zitto ambaye ni shabiki wa Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England pamoja na Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Dar es Salaam alisema: "Mimi nina wakati mgumu maana wakati wenzetu Yanga wanapanga mikakati ya ushindi Simba wanapigana na kupinduana, jana nilitarajia Liverpool watatupa ahueni kidogo lakini wametoka sare."
Alitoa kauli
hiyo kutokana na mgogoro uliopo Simba kati ya kamati ya utendaji na Mwenyekiti, Ismail Aden Rage na kuhusu Liverpool iliyoambulia sare ya 3-3 na Everton.

Zitto pia alisisitiza azma yake ya kutojitoa Chadema katika mkutano ambao pia ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, wengi wakiwa ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma kama ilivyo kwa Zitto.
Wasanii hao walichukua jukumu la kuwakaribisha waandishi wa habari katika mkutano huo ni pamoja na Afande Sele', Peter Msechu, Mwasiti, Queen Darlin na Baba Levo. Chanzo: Mwananspoti

No comments:

Post a Comment