Pages

Saturday, December 7, 2013

AKATWA PANGA KICHWANI NA KUPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA


a225Diwani-AthumaniTAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA
HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE  07.12. 2013.
WILAYA YA KYELA  -  MAUAJI.
MNAMO TAREHE 06.12.2013 MAJIRA YA SAA 00:01HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUBAGA, KATA YA  BUJONDE, TARAFA YA  UNYAKYUSA, WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA.  JAPHET S/O MWANGOLWA, MIAKA 83, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUBAGA ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI. MBINU NI KUMVIZIA MHANGA AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE NA MKE WAKE KISHA KUMUUA. CHANZO NI UGOMVI WA UKOO KUGOMBEA MASHAMBA YA  URITHI. WATUHUMIWA WATATU WALITAMBULIWA NA MKE WA MAREHEMU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. ALIPIPI S/O MWANGOLWA, MIAKA 77, KYUSA, MKULIMA [AMBAYE NI MDOGO WAKE NA MAREHEMU]   2. ANASTAZIA D/O NSOKA, MIAKA 40, KYUSA, MKULIMA [MKE WA MTUHUMIWA] 3. EVARIST  S/O ALIPIPI ULIMBOKA, MIAKA 30, KYUSA, FUNDI UMEME [MTOTO WA WATUHUMIWA] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA LUBAGA – BUJONDE.
TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MATATIZO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO NA KUJENGA HOJA BADALA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA PIA KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA KATIKA JAMII.
 [ BARAKAEL MASAKI   - ACP ]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment