Ramsey hakutaka kushangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani
ARSENAL imezidi kijichimbia kileleni
mwa Ligi Kuu ya England, baada ya kuilaza mabao 3-0 Cardiff City, kwenye
Uwanja wa Cardiff jioni hii.Mabao ya Arsenal yamefungwa na Aaron Ramsey dakika ya 29 akimalizia pasi ya Mesut Ozil na 90 pasi ya Theo Walcott na Mathieu Flamini dakika ya 86 pasi ya Ozil tena.
Ushindi huo, unaifanya Arsenal itemize pointi 31 baada ya kucheza mechi 13, ikiizidi Liverpool iliyo katika nafasi ya pili kwa pointi saba.
Lukaku akishangilia bao lake leo
Katika mechi nyingine za Ligi Kuu England leo,Everton imeichapa 4-0 Stoke City Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, mabao ya Gerard Deulofeu dakika ya 45, pasi ya Gareth Barry, Seamus Coleman dakika ya 49 pasi ya Barry tena, Bryan Oviedo dakika ya 58, pasi ya Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku dakika ya 79 pasi ya Oviedo.
Bao pekee la Gary Hooper dakika ya 30 limeipa Norwich ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Carrow Road, Norwich, Norfolk.
West HamUnited imeifunga 3-0 Fulham Uwanja wa Boleyn Ground, London mabao ya Mohamed Diame dakika ya 47, Carlton Michael Cole Okirie dakika ya 82 na Joe Cole dakika ya 88.
Aston Villa imetoka sare ya bila kufungana na Sunderland Uwanja wa Villa Park na mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England, Newcastle United imeifunga West Bromwich 2-1
No comments:
Post a Comment